Kitabu hiki kinaelezea elimu ya fedha na uwekezaji ili kuhamasisha wasomaji kuwa wawekezaji. Utajifunza jinsi ya kupanga na kuandaa bajeti ya fedha zako; nidhamu ya matumizi ya fedha; kuandaa mpango binafsi wa fedha na uwekezaji (wenye dira, dhamira, malengo, mpangokazi, mikakati n.k.). Utajifunza kuhusu hisa, faida na vivutio vilivyotolewa na Serikali kwa kumiliki hisa, vipande, hatifungani; maana na umuhimu wa masoko ya hisa; maneno yanayotumika katika masoko ya hisa; tofauti ya bei na thamani; utaratibu wa kununua na kuuza hisa; maana ya akiba, faida ya kuwa na akiba, jinsi ya kutenga akiba; faida ya kuwekeza/kulimbikiza; maana ya uwekezaji, vigezo muhimu vya kuzingatia kabla ya kutoa fedha na kuiweka katika biashara, kitegauchumi, hisa, vipande na hatifungani; taarifa ya mwaka;, uchambuzi wa taarifa za fedha; maana ya utawala bora, kanuni na vigezo vya uongozi na utawala bora katika kuendesha biashara na taasisi; tofauti ya mwekezaji na mviziaji; uamuzi wa aina nne katika uwekezaji; falsafa, mbinu na mikakati ya uwekezaji mahiri, makosa katika uwekezaji, jinsi ya kujenga tabia ya kuwa na akiba na kuwekeza, na changamoto katika uwekezaji.
Katuni, picha na hadithi mbalimbali, fupi na nzuri zitakuburudisha na kukuelimisha. Ujuzi ulioandikwa ndani ya kitabu hiki unalenga kuhamasisha msomaji kuwa mwekezaji. “Mfanyakazi, mwanafunzi, mjasiriamali, mwanataaluma unaweza kuwa mwekezaji makini”.