Eunice Mpezeni > Eunice's Quotes

Showing 1-30 of 56
« previous 1
sort by

  • #1
    Enock Maregesi
    “Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine.”
    Enock Maregesi

  • #2
    Enock Maregesi
    “Situmii madawa ya kulevya. Madawa ya kulevya ni mimi mwenyewe; nahitaji kusaidiwa!”
    Enock Maregesi

  • #3
    Enock Maregesi
    “Kuwa tajiri si kazi rahisi. Ukipata milioni ya kwanza utataka nyingine kulinda hiyo ya kwanza. Ukipata ya pili utataka mbili zingine kulinda hizo mbili za kwanza, n.k. Si kazi rahisi. Si kama unavyofikiria. Utajiri haujanipa furaha. Umenipa uhuru. Ndugu zangu ni maskini wa kutupwa. Ningependa kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi.”
    Enock Maregesi

  • #4
    Enock Maregesi
    “Heri kuwa maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka.”
    Enock Maregesi

  • #5
    Enock Maregesi
    “Kitu cha kwanza kufanya kama umeamua kuficha ukweli wape watu ukweli mwingine kulinda thamani ya utu wako.”
    Enock Maregesi

  • #6
    Enock Maregesi
    “The best prize life has to offer is not a chance to work hard and be something in the community. It is the perfume of God that resides within you.”
    Enock Maregesi
    tags: peace

  • #7
    Enock Maregesi
    “Mwalimu Julius Nyerere was a father to his family. To Tanzania he was a defender of a dream.”
    Enock Maregesi
    tags: legend

  • #8
    Enock Maregesi
    “Two plus two is not sometimes equal to four ... It is equal to four plus one because one is a powerful amalgamation.”
    Enock Maregesi

  • #9
    Enock Maregesi
    “Mojawapo ya misingi ya ujasusi ni kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya unachojua, usichojua na unachofikiria. Unaweza kusema unajua wakati hujui. Maamuzi yasiyo sahihi ya kijasusi huweza kuiletea tume madhara makubwa.”
    Enock Maregesi

  • #10
    Enock Maregesi
    “Katika jiji la Dar watu hawaendi kazini. Wanakwenda vitani. Wania kilicho chako ukidhulumiwa. Utajiri humpendelea anayejaribu.”
    Enock Maregesi
    tags: life

  • #11
    Enock Maregesi
    “Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa.”
    Enock Maregesi

  • #12
    Enock Maregesi
    “Heri kufuta mashtaka kuliko kumfunga mtuhumiwa asiyekuwa na makosa. Kuonewa kunauma.”
    Enock Maregesi

  • #13
    Enock Maregesi
    “Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta.”
    Enock Maregesi

  • #14
    Enock Maregesi
    “Usalama wa Taifa ni akili si ukali. Kazi yake, au wajibu wake; ni kukusanya, kuchanganua, kudurusu na kuunganisha kwa makini, taarifa nyeti za kijasusi za ndani na nje ya nchi kuilinda Tanzania na watu wake. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa tajiri kuwa tajiri wa unyenyekevu.”
    Enock Maregesi

  • #15
    Enock Maregesi
    “Serikali haifungi mtu kutokana na shinikizo la watu. Inafunga mtu kutokana na sheria za nchi.”
    Enock Maregesi

  • #16
    Enock Maregesi
    “Msichana wa miaka 18 miaka ya 70 ni sawa na msichana wa miaka 8 leo. Msichana wa miaka 8 leo anayajua maisha kuliko msichana wa miaka 18 miaka ya 70. Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa.”
    Enock Maregesi

  • #17
    Enock Maregesi
    “Uraibu ni mbaya unapoathiri maisha ya mtu.”
    Enock Maregesi

  • #18
    Enock Maregesi
    “Kucheza muziki si lazima utingishe mwili kama mwendawazimu. Unaweza kucheza kwa hisia.”
    Enock Maregesi

  • #19
    Enock Maregesi
    “Utakapofika mwisho wa njia, geuka. Huo ndiyo mwanzo wa njia nyingine.”
    Enock Maregesi

  • #20
    Enock Maregesi
    “Jibu nilichokuuliza. Utajibu, hutajibu?"
    "Nitajibu."
    "Usipojibu?"
    "Nitajipaka rangi, ya pinki." Murphy hakumwelewa.
    "Utanifanya chochote utakachotaka."
    "Mmenigundua vipi?" Murphy aliuliza akirekebisha suruali.”
    Enock Maregesi

  • #21
    Enock Maregesi
    “Addiction isn't about using drugs. It's about what the drug does to your life.”
    Enock Maregesi

  • #22
    Enock Maregesi
    “Joram Kiango ni mpelelezi maarufu nchini Tanzania. Willy Gamba ni mpelelezi maarufu katika bara la Afrika. John Murphy ni mpelelezi maarufu duniani. Ni watu watatu tofauti wanaofanya kazi zinazofanana.”
    Enock Maregesi

  • #23
    Enock Maregesi
    “Kolonia Santita ni tofauti na hadithi zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.”
    Enock Maregesi

  • #24
    Enock Maregesi
    “Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawaoni unachokiona. Ndoto yako waijua mwenyewe.”
    Enock Maregesi

  • #25
    Enock Maregesi
    “Kinachotokea leo kitatuathiri kesho. Mbegu tunazopanda sasa ni mazao ya msimu ujao.”
    Enock Maregesi

  • #26
    Enock Maregesi
    “Mungu alitupa masikio mawili na ulimi mmoja. Tunatakiwa kusikiliza zaidi kuliko kuongea.”
    Enock Maregesi

  • #27
    Enock Maregesi
    “Usipobadilisha maisha yako maisha yako yatakubadilisha.”
    Enock Maregesi

  • #28
    Enock Maregesi
    “Gari ya Debbie huchukua sekunde 12 kutoka kilometa 0 mpaka kilometa 210 kwa saa. Huchukua sekunde 10 kutoka kilometa 210 kwa saa mpaka kilometa 0. Ina uwezo wa kusimama haraka kuliko inavyoweza kukimbia.”
    Enock Maregesi

  • #29
    Enock Maregesi
    “Mtu aliyepoteza kazi na mke na watoto wake kuuwawa kwa mfano, watu wanapaswa kuwa makini na yeye, ana uwezo wa kufanya chochote.”
    Enock Maregesi

  • #30
    Enock Maregesi
    “Mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake ana uwezo wa kufanya chochote.”
    Enock Maregesi



Rss
« previous 1