Phoebe Majigo > Phoebe's Quotes

Showing 1-30 of 124
« previous 1 3 4 5
sort by

  • #1
    Enock Maregesi
    “Kujiingiza katika madawa ni matokeo ya maisha. Hatutumii madawa ya kulevya. Madawa ya kulevya ni sisi wenyewe; tunahitaji kusaidiwa.”
    Enock Maregesi

  • #2
    Enock Maregesi
    “Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa.”
    Enock Maregesi

  • #3
    Enock Maregesi
    “Kuwa tajiri si kazi rahisi. Ukipata milioni ya kwanza utataka nyingine kulinda hiyo ya kwanza. Ukipata ya pili utataka mbili zingine kulinda hizo mbili za kwanza, n.k. Si kazi rahisi. Si kama unavyofikiria. Utajiri haujanipa furaha. Umenipa uhuru. Ndugu zangu ni maskini wa kutupwa. Ningependa kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi.”
    Enock Maregesi

  • #4
    Enock Maregesi
    “The best prize life has to offer is not a chance to work hard and be something in the community. It is the perfume of God that resides within you.”
    Enock Maregesi
    tags: peace

  • #5
    Enock Maregesi
    “Serikali haifungi mtu kutokana na shinikizo la watu. Inafunga mtu kutokana na sheria za nchi.”
    Enock Maregesi

  • #6
    Enock Maregesi
    “Uraibu ni mbaya unapoathiri maisha ya mtu.”
    Enock Maregesi

  • #7
    Enock Maregesi
    “Heri kuwa maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka.”
    Enock Maregesi

  • #8
    Enock Maregesi
    “Mihadarati ni chanzo kikubwa cha matatizo ya wanadamu. Mshahara wake ni wazimu, uhalifu na mauti.”
    Enock Maregesi

  • #9
    Enock Maregesi
    “Kufanya kosa huku ukijua ni kosa ni kujiombea jela mwenyewe.”
    Enock Maregesi

  • #10
    Enock Maregesi
    “Joram Kiango ni mpelelezi maarufu nchini Tanzania. Willy Gamba ni mpelelezi maarufu katika bara la Afrika. John Murphy ni mpelelezi maarufu duniani. Ni watu watatu tofauti wanaofanya kazi zinazofanana.”
    Enock Maregesi

  • #11
    Enock Maregesi
    “Vichwa vitatu vya sururu na chembe tatu za bunduki za Kalashnikov; na alama ya bahati, mafanikio, udhalimu na mwanzo mpya ya msalaba wa swastika, kama alama ya ujenzi na uhalifu wa Kolonia Santita.”
    Enock Maregesi

  • #12
    Enock Maregesi
    “Kolonia Santita ni tofauti na hadithi zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.”
    Enock Maregesi

  • #13
    Enock Maregesi
    “Kucheza muziki si lazima utingishe mwili kama mwendawazimu. Unaweza kucheza kwa hisia.”
    Enock Maregesi

  • #14
    Enock Maregesi
    “Kujamiiana si anasa tena katika maisha yangu. Ni hitaji muhimu kwa ujenzi wa familia.”
    Enock Maregesi

  • #15
    Enock Maregesi
    “Mapenzi ni kiburudisho kikubwa kuliko vyote katika maisha.”
    Enock Maregesi

  • #16
    Enock Maregesi
    “Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu.”
    Enock Maregesi

  • #17
    Enock Maregesi
    “Kila mtu hapa duniani ni jirani yako. Hakuna mtu mwingine hapa ulimwenguni isipokuwa sisi. Lazima tujifunze kuishi pamoja.”
    Enock Maregesi

  • #18
    Enock Maregesi
    “Kikamilikacho si kiimarishwacho.”
    Enock Maregesi

  • #19
    Enock Maregesi
    “Fikiria kwanza maana ya unachosema. Halafu sema.”
    Enock Maregesi

  • #20
    Enock Maregesi
    “Neno moja kutoka mdomoni mwako linaweza kukuletea madhara makubwa. Fikiria kwanza maana ya kitu unachofikiria (ambacho tayari umekisema kichwani mwako) kabla ya kukisema tena mdomoni mwako. Wenye hekima huzungumza kwa sababu wana kitu cha kuzungumza. Wapumbavu hubwabwaja.”
    Enock Maregesi

  • #21
    Enock Maregesi
    “Kushukuru wakati wa matatizo ni kafara ya maombi.”
    Enock Maregesi

  • #22
    Enock Maregesi
    “Kigumu kuliko vyote ni kizuri kuliko vyote.”
    Enock Maregesi

  • #23
    Enock Maregesi
    “Nitajisikia raha sana kufungwa kwa ajili ya matatizo watu.”
    Enock Maregesi

  • #24
    Enock Maregesi
    “Kupata kitu ambacho hujawahi kupata lazima ufanye kitu ambacho hujawahi kufanya.”
    Enock Maregesi

  • #25
    Enock Maregesi
    “Kama huwezi kumpenda mtu usimchukie.”
    Enock Maregesi

  • #26
    Enock Maregesi
    “Kuikaribisha amani ya Mungu katika maisha yangu kumenisaidia. Naishi mbinguni duniani.”
    Enock Maregesi

  • #27
    Enock Maregesi
    “Kadiri unavyozidi kupanda juu ndivyo utakavyoanguka vibaya.”
    Enock Maregesi

  • #28
    Enock Maregesi
    “Ukitaka kuwa mfanyabiashara mzuri wa madawa ya kulevya usitumie madawa ya kulevya. Siri ya mafanikio ya Kolonia Santita ni nidhamu na kitalifa.”
    Enock Maregesi

  • #29
    Enock Maregesi
    “Addiction isn't about using drugs. It's about what the drug does to your life.”
    Enock Maregesi

  • #30
    Enock Maregesi
    “Usalama wa Taifa ni akili si ukali. Kazi yake, au wajibu wake; ni kukusanya, kuchanganua, kudurusu na kuunganisha kwa makini, taarifa nyeti za kijasusi za ndani na nje ya nchi kuilinda Tanzania na watu wake. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa tajiri kuwa tajiri wa unyenyekevu.”
    Enock Maregesi



Rss
« previous 1 3 4 5