,

Falsafa Quotes

Quotes tagged as "falsafa" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Nilijifunza toka awali umuhimu wa kushindwa katika maisha ijapokuwa nilijitahidi sana, na nilipoendelea kushindwa niliweka nadhiri ya kufanya kitu kimoja kilicholeta maana zaidi katika maisha yangu nacho ni uandishi wa vitabu. Uandishi wa vitabu ndicho kitu pekee nilichokiweza zaidi kuliko vingine vyote na kuanzia hapo Mungu aliniweka huru. Nilijua mimi ni nani. Nilijua kwa nini nilizaliwa. Nilijifunza falsafa ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko nilivyoikuta – kwa sababu hata mimi nilikuwepo – na falsafa ya kushindwa si hiari. Maarifa hayo yakafanya niwe na heshima na upendo kwa watu wote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kitalifa ni utiifu kamili, woga, umbali (kwa maana ya kuwa mbali na biashara ya mamafia wengine mpaka kwa makubaliano maalumu) na nidhamu ya kutoshirikiana na mamlaka zote za serikali. Ukishtakiwa kwa kosa la madawa au ujambazi ambalo hukufanya, utatumikia kifungo mpaka mwisho bila kushirikiana na polisi (kwa maana ya kutaja aliyehusika au waliohusika na uhalifu huo) hata kama aliyehusika au waliohusika hana au hawana uhusiano wowote na Kolonia Santita. Falsafa ya Kitalifa ni Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita. Na adhabu ya kuvunja sheria hiyo ni kifo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sina jinsi. Nguzo ya maisha yangu ni historia ya maisha yangu. Historia ya maisha yangu ni urithi wa watu waliojifunza kusema hapana kwa ndiyo nyingi – waliojitolea vitu vingi katika maisha yao kunifikisha hapa nilipo leo – walionifundisha falsafa ya kushindwa si hiari. Siri ya mafanikio yangu ni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu wote. Hiyo wote katika herufi kubwa.

Wote katika herufi kubwa (WOTE) si neno la kawaida falau katika nukuu hii ya mafanikio. Linamaanisha kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote uliopewa na Mwenyezi Mungu. Watu wengi hujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao. Usijitahidi kwa kadiri ya uwezo wako. Jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE.”
Enock Maregesi