Hypovolemic Shock Quotes

Quotes tagged as "hypovolemic-shock" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Damu na maji vilitoka katika mbavu za Yesu Kristo kutokana na upungufu wa damu mwilini, hipovolimia, kulikotokana na kuchapwa bakora. Yesu alichapwa bakora arobaini kabla ya kupelekwa Golgotha. Matokeo ya hipovolimia katika mwili wa mtu ni moyo kwenda mbio kusukuma damu iliyopungua, kuzimia kutokana na msukumo wa damu kuwa chini, figo kushindwa kufanya kazi na kiu ya maji.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna ushahidi wa kutosha katika maandiko kwamba Yesu aliugua hipovolimia kutokana na kuchapwa. Yesu alipobeba msalaba wake kuelekea Golgotha alianguka, na mtu mmoja aliyeitwa Simoni alilazimishwa ama kuubeba au kumsaidia Yesu kuubeba msalaba huo hadi kilimani. Kuanguka huko kunaonyesha kwamba Yesu alikuwa na shinikizo la damu. Alama nyingine inayoonyesha kwamba Yesu alipatwa na ugonjwa wa hipovolimia ni pale alipodai kuwa alikuwa na kiu, akiwa msalabani, akimaanisha kiu ya maji.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kabla ya kukata roho mapigo ya kasi ya moyo aliyoyapata Yesu kutokana na mshtuko wa hipovolimia, pia yalisababisha maji kujikusanya katika vifuko vya maji au ute kandokando ya moyo na kandokando ya mapafu. Mkusanyiko huu wa maji kandokando ya moyo hujulikana kama ‘pericardial effusion’ na mkusanyiko wa maji kandokando ya mapafu hujulikana kama ‘pleural effusion’. Hii ndiyo maana baada ya Yesu kukata roho, na askari wa Kirumi kurusha mkuki katika ubavu wake, baada ya kutoboa mapafu na moyo, damu na maji vilitoka katika mbavu za Yesu kama Yohana alivyorekodi katika Injili yake. Mapafu ya Yesu na tumbo la Yesu vilijaa damu na maji. Mkuki ulivyotupwa maji yalitoka katika mapafu ya Yesu na katika tumbo la Yesu, na katika utando unaozunguka moyo wa Yesu, kutokana na kupasuka kwa moyo.”
Enock Maregesi