,

Manabii Wa Uongo Quotes

Quotes tagged as "manabii-wa-uongo" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Manabii wa uongo, na wafuasi wao, hawautaki ukweli. Kazi yao ni kutulazimisha tumwabudu Mpinga Kristo, badala ya Yesu Kristo, bila sisi wenyewe kujua. Wana mamlaka yote ya Mpinga Kristo kwa sababu, kama Mpinga Kristo, wanaongozwa na Shetani. Walimu hawa wa uongo wanaopenda kuvalia misurupwenye ya kisawasawa, na wanaoongea utafikiri wamemeza Biblia na kuitapika kwenye mikrofoni, lengo lao ni kutupeleka kwenye ufalme wa Shetani. Hatuna budi kuitangaza injili ya kweli ya Yesu Kristo, kwa imani ya kweli, kupata urithi usiohongeka wa ufalme wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Manabii wa uongo wana dhambi kuu tatu: tamaa ya ngono, uasi dhidi ya mamlaka ya Kristo, na dharau kwa Shetani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Utii kwa Mungu unapokosekana injili ambayo Mungu anataka ihubiriwe haitahubiriwa. Itahubiriwa na manabii wa uongo.”
Enock Maregesi