Mwanasheria Quotes

Quotes tagged as "mwanasheria" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Dikteta uchwara ni sifa nzuri na Lissu analijua hilo kwa sababu yeye ni mwanasheria, na JPM analijua hilo kwa sababu yeye ni Rais wa nchi. Rais ni alama ya utulivu wa nchi. Hatima ya Lissu iko mikononi mwa JPM.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kwa nini mtoto mchanga anapokuwa ananyonya ziwa la mama yake, mara nyingi humwangalia mama yake machoni? Kwa sababu, licha ya macho kuonekana kitu cha ajabu kwake, mtoto mchanga, bila kujitambua, hutamani sana mama yake amwambie neno zuri atakalolitumia baadaye katika maisha yake atakapokuwa mkubwa. Maneno huumba. Ukimwambia mwanao kuwa anaonekana atakuwa jambazi, anaweza kuwa jambazi kweli atakapokuwa mkubwa; ukimwambia kuwa anaonekana atakuwa mwanasheria, anaweza kuwa mwanasheria kweli atakapokuwa mkubwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama ulikuwa ukimwambia mwanao kuwa atakuwa jambazi labda kwa sababu ya fujo zake alipokuwa mdogo, mambo mengi atakayokuwa anayafikiria au anayaota atakapopevuka akili ni ya kihalifu. Kwani hayo ndiyo mambo ya kwanza kabisa kujirekodi katika ubongo wake alipokuwa hajitambui. Lakini kama ulikuwa ukimwambia kuwa atakuwa daktari au mwanasheria, mambo mengi atakayokuwa anayafikiria au anayaota ni ya kidaktari au kisheria. Kuna uwezekano mkubwa akawa daktari au mwanasheria baadaye katika maisha yake.”
Enock Maregesi