They Deserve Quotes

Quotes tagged as "they-deserve" Showing 1-2 of 2
Enock Maregesi
“Msamaha si jambo rahisi. Tunapoumizwa, au watu wetu wa karibu wanapoumizwa, tendo la kusamehe linaweza kuwa gumu kuliko matendo yote. Lakini, tambua kwamba msamaha ni mchakato wa muda mrefu unaohitaji ujasiri mkubwa kuuanza hadi kuukamilisha, ongea na watu wanaoelewa maana ya msamaha ili wakuongoze katika mchakato huo. Vilevile, tambua kwamba hata wewe umewahi kufanya makosa na unahitaji msamaha, tambua kwamba suluhisho kamili linahitaji matendo kutoka kwa aliyekosea na kwa aliyekosewa. Wengine hupendwa kwa sababu wanastahili, lakini wengine wanastahili kwa sababu hupendwa. Mungu anatupenda kwa jinsi tulivyo hata kama tunajiona hatustahili. Hivyo, jithamini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.”
Enock Maregesi