Usikate Tamaa Quotes

Quotes tagged as "usikate-tamaa" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Usikate tamaa juu ya ndoto zako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“ATP hutumika katika kipindi ambapo mtu anakuwa amekata tamaa kabisa katika jambo lolote analolifanya, na yeyote anayetumia ATP ana uwezo mkubwa wa kufanikiwa katika maisha yake. Hivyo, usikate tamaa, jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Marafiki wanaweza kukupotosha bila wao wenyewe kujua na bila kuwa na nia mbaya ya aina yoyote ile; na wanaweza kuwa washauri wazuri kwa sababu wanakujua vizuri unapokuwa na huzuni, na wanakujua vizuri unapokuwa na furaha pia. Kwa mfano; rafiki yako anaweza kukushauri kusomea uhasibu wakati Mungu amekupangia utawala, au anaweza kujua aongee na wewe wakati gani kulingana na tabia yako ya kubadilikabadilika. Maadui wanasaidia kujua kipaji ulichopewa na Mungu – ukifanya kitu ambacho si cha kawaida katika maisha yako halafu ukawa na maadui ujue hicho ndicho Mungu alichokupangia kufanya, hivyo usikate tamaa – na mashabiki wanasaidia kufanya kipaji chako kiwe na uhai.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Abra maana yake ni fursa. Kwa hiyo, geuza matatizo yako kuwa fursa. Lakini, utageuzaje matatizo yako kuwa fursa? Kugeuza matatizo yako kuwa fursa, amini kama unaweza, usitumie muda mwingi kufikiria tatizo, tumia muda mwingi kufikiria fursa. Ukipata tatizo usikate tamaa. Badala yake, geuza tatizo hilo kuwa faida.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Usikate tamaa kabla ya kufa. Pambana.”
Enock Maregesi