Afrika Mashariki Quotes

Quotes tagged as "afrika-mashariki" Showing 1-5 of 5
Enock Maregesi
“Kiswahili ni lugha rasmi ya nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Ni lugha isiyo rasmi ya nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lugha ya Kiswahili ni mali ya nchi za Afrika ya Mashariki, si mali ya nchi za Afrika Mashariki peke yake. Pia, Kiswahili ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika; pamoja na Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kihispania. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote ile, duniani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kiswahili ni lugha ya Kibantu na lugha kuu ya kimataifa ya biashara ya Afrika ya Mashariki ambayo; maneno yake mengi yamepokewa kutoka katika lugha za Kiarabu, Kireno, Kiingereza, Kihindi, Kijerumani na Kifaransa, kutoka kwa wakoloni waliyoitawala pwani ya Afrika ya Mashariki katika kipindi cha karne tano zilizopita.

Lugha ya Kiswahili ilitokana na lugha za Kisabaki za Afrika Mashariki; ambazo nazo zilitokana na Lugha za Kibantu za Pwani ya Kaskazini Mashariki za Tanzania na Kenya, zilizotokana na lugha zaidi ya 500 za Kibantu za Afrika ya Kusini na Kati.

Lugha za Kibantu zilitokana na lugha za Kibantoidi, ambazo ni lugha zenye asili ya Kibantu za kusini mwa eneo la Wabantu, zilizotokana na jamii ya lugha za Kikongo na Kibenue – tawi kubwa kuliko yote ya familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri katika bara la Afrika. Familia ya lugha za Kikongo na Kibenue ilitokana na jamii ya lugha za Kiatlantiki na Kikongo; zilizotokana na familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri, ambayo ni familia kubwa ya lugha kuliko zote duniani kwa maana ya lugha za kikabila.

Familia ya lugha ya Kiswahili imekuwepo kwa karne nyingi. Tujifunze kuzipenda na kuzitetea lugha zetu kwa faida ya vizazi vijavyo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini Kiswahili kilizaliwa Afrika Mashariki. Kwa nini hatuithamini lugha yetu? Kwa nini hatuzithamini lugha zetu za makabila? Kwa nini hatuipendi na kuitetea lugha yetu ya taifa ambayo ndiyo lugha ya biashara na mawasiliano ya Afrika Mashariki? Kwa nini hatuvitetei vizazi vijavyo kwa kuvitetea vizazi vya leo?”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kiingereza kilipanda meli na ndege kutoka Uingereza kuja Afrika Mashariki. Tujivunie Kiswahili chetu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kiingereza kililetwa na wakoloni wa Kiingereza kutoka Uingereza na walikitumia katika masuala yote ya kiutawala ya Afrika Mashariki. Kililetwa pia na wamisionari waliojenga shule na kuwafundisha Kiingereza wanafunzi na walimu na watu wengine wa kawaida, kwa lengo la kuwasaidia katika kazi yao ya kueneza dini kama wakalimani, hivyo kufanya Kiingereza kienee zaidi kuliko Kiswahili.”
Enock Maregesi