Kiswahili Quotes
Quotes tagged as "kiswahili"
Showing 1-9 of 9
“Kiswahili ni lugha rasmi ya nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Ni lugha isiyo rasmi ya nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lugha ya Kiswahili ni mali ya nchi za Afrika ya Mashariki, si mali ya nchi za Afrika Mashariki peke yake. Pia, Kiswahili ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika; pamoja na Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kihispania. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote ile, duniani.”
―
―
“Kiswahili ni lugha ya Kibantu na lugha kuu ya kimataifa ya biashara ya Afrika ya Mashariki ambayo; maneno yake mengi yamepokewa kutoka katika lugha za Kiarabu, Kireno, Kiingereza, Kihindi, Kijerumani na Kifaransa, kutoka kwa wakoloni waliyoitawala pwani ya Afrika ya Mashariki katika kipindi cha karne tano zilizopita.
Lugha ya Kiswahili ilitokana na lugha za Kisabaki za Afrika Mashariki; ambazo nazo zilitokana na Lugha za Kibantu za Pwani ya Kaskazini Mashariki za Tanzania na Kenya, zilizotokana na lugha zaidi ya 500 za Kibantu za Afrika ya Kusini na Kati.
Lugha za Kibantu zilitokana na lugha za Kibantoidi, ambazo ni lugha zenye asili ya Kibantu za kusini mwa eneo la Wabantu, zilizotokana na jamii ya lugha za Kikongo na Kibenue – tawi kubwa kuliko yote ya familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri katika bara la Afrika. Familia ya lugha za Kikongo na Kibenue ilitokana na jamii ya lugha za Kiatlantiki na Kikongo; zilizotokana na familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri, ambayo ni familia kubwa ya lugha kuliko zote duniani kwa maana ya lugha za kikabila.
Familia ya lugha ya Kiswahili imekuwepo kwa karne nyingi. Tujifunze kuzipenda na kuzitetea lugha zetu kwa faida ya vizazi vijavyo.”

“Lakini Kiswahili kilizaliwa Afrika Mashariki. Kwa nini hatuithamini lugha yetu? Kwa nini hatuzithamini lugha zetu za makabila? Kwa nini hatuipendi na kuitetea lugha yetu ya taifa ambayo ndiyo lugha ya biashara na mawasiliano ya Afrika Mashariki? Kwa nini hatuvitetei vizazi vijavyo kwa kuvitetea vizazi vya leo?”
―
―
“Wajerumani, hata hivyo, wakati wa utawala wao waliruhusu Kiswahili kiwe lugha halisi ya taifa nchini Tanzania kwa vile hawakukiongea Kiingereza wala hawakukipenda. Ndiyo maana Kiswahili kinazungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko Kenya au Uganda.”
―
―
“Andika Kiswahili vizuri. Wala usiogope kuonekana mshamba. Kwa sababu unachokifanya hasa ni kwa ajili ya vizazi vijavyo.”
―
―
“Komandoo Nicolas Kahima Kankiriho ('Kahima the Warrior') alizaliwa katika Wilaya ya Bushenyi, Ankole, kusini-magharibi mwa Uganda, Julai 24, 1954, mtoto wa tano kuzaliwa, katika familia ya watoto sita ya Nicodemas Kankiriho; mzee wa heshima wa Wabaima, aliyekuwa akisifika sana kwa uchungaji (wa mifugo) na msisitizo mkali wa ukiristo kwa watoto wake wote; hasa Kahima na Yebare, binti yake wa pekee, aliyekuwa wa mwisho kuzaliwa.
Kahima (futi 6 inchi 3 aliyekuwa akiongea Kinyankole, Kiswahili, Kiingereza na Kihispania kwa ufasaha), baada ya kutoka Uganda – kwa mafunzo ya mwanzo ya ukomandoo ya Kiisraeli – alikwenda Urusi na Korea ya Kaskazini ambako aliongeza ujuzi hadi kiwango cha juu kabisa; kabla ya kwenda Amerika ya Kusini, kama askari wa msituni wa vyama vya kisiasa visivyo rasmi vya magorila wa Kolombia.
Akiwa Kolombia, Kahima alikutana na Eduardo Chapa de Christopher (kiongozi wa zamani wa Kateli ya Diablos de Amazonas, Mashetani wa Amazoni, iliyokuwa ikivilinda vyama vya kisiasa vya magorila vya Americas) ambaye alimwajiri kama mlinzi binafsi na baadaye kama mlinzi binafsi wa Carlos Pulecio Alcántara – kiongozi wa kwanza wa Kateli ya Kolonia Santita. Alcántara alipouwawa, Kahima alihamia kwa Panthera Tigrisi – Kiongozi Mkuu wa Kolonia Santita.”

“Kiingereza kililetwa na wakoloni wa Kiingereza kutoka Uingereza na walikitumia katika masuala yote ya kiutawala ya Afrika Mashariki. Kililetwa pia na wamisionari waliojenga shule na kuwafundisha Kiingereza wanafunzi na walimu na watu wengine wa kawaida, kwa lengo la kuwasaidia katika kazi yao ya kueneza dini kama wakalimani, hivyo kufanya Kiingereza kienee zaidi kuliko Kiswahili.”
―
―
“Hata wamisionari, hasa wamisionari wa Kiprotestanti, hawakukitumia Kiingereza katika kueneza dini kwa sababu hadhira yao isingewaelewa. Badala yake walitumia lugha za makabila ya Kiswahili, hivyo kujikuta wakieneza zaidi utamaduni wa Kiswahili kuliko wa Kiingereza au Kijerumani.”
―
―
All Quotes
|
My Quotes
|
Add A Quote
Browse By Tag
- Love Quotes 102k
- Life Quotes 80k
- Inspirational Quotes 76.5k
- Humor Quotes 44.5k
- Philosophy Quotes 31k
- Inspirational Quotes Quotes 29k
- God Quotes 27k
- Truth Quotes 25k
- Wisdom Quotes 25k
- Romance Quotes 24.5k
- Poetry Quotes 23.5k
- Life Lessons Quotes 23k
- Quotes Quotes 21k
- Death Quotes 20.5k
- Happiness Quotes 19k
- Hope Quotes 18.5k
- Faith Quotes 18.5k
- Inspiration Quotes 17.5k
- Spirituality Quotes 16k
- Relationships Quotes 15.5k
- Life Quotes Quotes 15.5k
- Motivational Quotes 15.5k
- Religion Quotes 15.5k
- Love Quotes Quotes 15.5k
- Writing Quotes 15k
- Success Quotes 14k
- Travel Quotes 14k
- Motivation Quotes 13.5k
- Time Quotes 13k
- Motivational Quotes Quotes 12.5k