Wamisri Quotes

Quotes tagged as "wamisri" Showing 1-2 of 2
Enock Maregesi
“Ukanda wa Gaza ni jimbo lenye miji minne na kambi mbalimbali za wakimbizi za Umoja wa Mataifa – lenye urefu wa kati ya kilometa 41 au maili 25 na lenye upana wa kati ya kilometa 6 mpaka 12 au maili 3.7 mpaka 7.5, pamoja na eneo la jumla la kilometa za mraba 365 au maili za mraba 141. Jimbo hili liliwahi kutawaliwa na Wamisri, Wakaanani, Waisraeli, Wasiria, Wababelonia, Wagiriki, Warumi, Waturuki, Waingereza, na Wapalestina, na limekuwa uwanja wa vita kwa karne nyingi kwa sababu za kidini na kihistoria. Ukanda wa Gaza uko chini ya Palestina. Uko chini ya serikali ya Hamas.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kwa vile taifa la Israeli lilipoteza haki yake ya upendeleo, Mungu aliahidi kuliharibu kama alivyoyaharibu mataifa ya Waamori na Wamisri. Watu wa Israeli walishafika mbali sana kiasi cha Mungu kutokutegemea tena toba kutoka kwao. Kuna muda wa fursa na kuna muda ambao fursa haipo tena. Nafasi ya Israeli ya kutubu ilishafikia mwisho.

Kama alivyokuwa amepigana vita vyao kwa ajili yao katika siku za nyuma sasa Mungu alipigana nao. Pamoja na ujasiri na utaalamu wao wote wasingependelewa tena. Mambo ambayo mwanzo yaliipa Israeli nguvu katika vita yaliwageukia.”
Enock Maregesi