Adamu Na Hawa Quotes

Quotes tagged as "adamu-na-hawa" Showing 1-6 of 6
Enock Maregesi
“Tunazaliwa, kuteseka na kufa kwa sababu ya dhambi ya asili ya wazazi wetu wa kwanza (Adamu na Hawa). Kama Hawa asingekubali kudanganywa na Shetani, tungezaliwa bila uchungu, tungeishi bila kuteseka na tusingekufa milele. Lakini haya ndiyo mawazo yangu: Mungu Ahusiki na dhambi, Ahusiki na mwili, Anahusika na roho. Hivyo, mtu anapofariki mwili unabaki duniani lakini roho inarudi kwa Mungu; kwani Yeye ndiye aliyeitengeneza na kuiweka katika moyo wa mtu. Mimi na wewe ni viumbe vyenye thamani kubwa sana mbele za Mwenyezi Mungu; mapenzi Yake kwetu hayana masharti yoyote. Hainiingii akilini (hata kidogo) kumtesa mtu unayempenda kiasi hicho milele, wakati uwezo wa kumwokoa unao.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dhambi ya Adamu ilileta mauti duniani (kwa viumbe vyote, si tu kwa binadamu). Hiyo ni kwa mujibu wa Biblia. Kisayansi si kweli; kwa sababu mauti yalikuwepo kabla Adamu na Hawa hawajaumbwa! Lakini haya ndiyo mawazo yangu: Dhambi iliathiri uumbaji wote ikiwemo mimea, wanyama, wadudu na kila kitu kilichoumbwa na Mwenyezi Mungu; ambavyo huteseka kwa sababu ya laana ya dunia. Kama wanyama na mimea visingekuwa vinakufa, binadamu wasingepata mahali pa kuishi. Hata hivyo, kifo cha Yesu msalabani kitafufua kila kitu – kitafufua uumbaji wote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani alikuwa kiumbe mzuri kuliko wote mbinguni na ulimwenguni. Mungu alimpendelea. Alikuwa mzuri kuliko malaika wote na alikuwa na nguvu kuliko kiumbe mwingine yoyote yule aliyeumbwa na Mungu, akiwemo binadamu. Lakini alipotupwa kutoka mbinguni kuja duniani kama Adamu na Hawa walivyotupwa kutoka bustanini kuja duniani, Shetani alipoteza sifa yake. Alipoteza sifa yake kwa sababu ya dhambi aliyoitenda, dhambi ya kiburi, na kwa sababu ya kuwa mbali na utukufu wa mbinguni. Badala ya kuwa kiumbe mzuri kuliko wote, Shetani akawa kiumbe mbaya kuliko wote. Mungu akaahidi kutokumsamehe, kwa sababu yeye ndiye kiumbe wa kwanza kutenda dhambi mbinguni na ulimwenguni, kwani hakushawishiwa na mtu kumuasi Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Damu, mto wa maisha unaotiririsha maji yake mwilini kwa kusukumwa na pampu za moyo na kuchujwa na fizi za mapafu, inaundwa na seli na maji yaitwayo utegili au maji ya damu, ambayo kazi yake ni kusafirisha oksijeni na virutubisho katika kila sehemu ya mwili, ndani yake kuna roho. Mungu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Ibrahimu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Israeli ijapokuwa mapenzi ya Mungu kwa Israeli yalikwisha baada ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Wana wa Israeli walitoa kafara za damu kwa ajili ya wokovu wa watoto wao wa kwanza na watoto wa kwanza wa wanyama wao nchini Misri. Mungu alitoa kafara ya damu ya Yesu Kristo nchini Israeli kwa ajili ya wanadamu wote duniani. Damu ya mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi, imetiwa wakfu na Mwenyezi Mungu na ina uhusiano mkubwa na ulimwengu wa roho. Ukifunikwa na damu ya mwanakondoo Shetani hatakuona. Shetani asipokuona, utafanikiwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Siku ya kwanza dhambi ya kwanza ilipotendwa Mungu alitoa kafara ya kwanza ya wanyama kwa ajili ya wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa. Adamu na Hawa walikuwa uchi, baada ya kutenda dhambi, Mungu akawalaani lakini akawapa uwezo wa muda mfupi wa kutubu dhambi zao ili awasamehe! Kutokana na ngozi za wanyama hao walipata mavazi na kutokana na damu ya wanyama hao walipata fursa ya kuishi na kutubu dhambi zote walizozitenda. Bila hivyo wasingepata muda wa kusamehewa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Adamu na Hawa walipotenda dhambi waligundua kuwa kumbe walikuwa na miili, walipogundua kuwa walikuwa uchi, kisha Mungu akawalaani. Miili yao ikakosa thamani mbele ya Mungu, sisi wote tukalaaniwa pamoja nao. Kwa Mungu hii miili haina thamani hata kidogo. Chenye thamani ni roho.”
Enock Maregesi