Mbinguni Quotes

Quotes tagged as "mbinguni" Showing 1-15 of 15
Enock Maregesi
“Kufanikiwa katika maisha lazima kitu fulani ambacho si cha kawaida kitokee katika maisha yako, bila kujali uko upande wa Yesu au upande wa Shetani. Kufanikiwa katika maisha ni sawa na kwenda mbinguni, au kuishi mbinguni duniani. Kitu ambacho si cha kawaida kutokea katika maisha yako ni sawa na kifo. Fanya kitu ambacho hujawahi kufanya kupata kitu ambacho hujawahi kupata.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani anaogopa viumbe saba tu hapa duniani na huko mbinguni ukimwondoa Mungu, ambaye anaogopwa na kila kiumbe: Malaika Mikaeli, Malaika Gabrieli, Malaika Rafaeli, Malaika Urieli, Malaika Selafieli, Malaika Ragueli, na Malaika Barakieli, ambao ni malaika wakuu; na tukio ambalo Shetani analiogopa zaidi ni tukio la kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili ambalo limekaribia sana, na atafanya kila atakachoweza kabla ya tukio hilo kuchukua roho zetu. Lengo la Shetani ni kuua kila mtu duniani kumkomoa Mungu na malaika wakuu na kutupeleka kuzimu. Lakini atashindwa kwa jina la Yesu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni uzima wa milele. Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni Shetani. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni Yesu Kristo. Yesu Kristo ni njia iliyo huru ya kwenda mbinguni. Shetani ni njia iliyo huru ya kwenda ahera.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani alikuwa malaika aliyeumbwa na Mungu lakini baadaye akamwonea Mungu wivu, wivu wa madaraka, hivyo Mungu akamtupa duniani kwa sababu ya kupingana na utawala wake mtakatifu. Duniani Shetani akamtumia nyoka kama mdakale kumdanganya Hawa. Hawa na Adamu wakamsikiliza Shetani badala ya kumsikiliza Mungu, nao wakalaaniwa. Shetani akajidai kuwa alikuwa na uwezo wa kufanya uzao wote wa Adamu na Hawa uwe mbali na Mungu, hivyo Mungu akampa muda wa kujaribu na kuthibitisha madai yake, lakini Shetani mpaka leo bado hajafanikiwa. Wakiitawala dunia leo kwa udanganyifu wa hali ya juu, pamoja naye, ni baadhi ya malaika ambao Shetani alifanikiwa kuwalaghai huko mbinguni. Mungu akawalaani pia na kuwatupa huku duniani, ambako Shetani alipapenda zaidi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Heri kuwa maskini kwa miaka mingi duniani na kuwa tajiri wa milele mbinguni kuliko kuwa tajiri kwa miaka mingi duniani na kuwa maskini wa milele ahera.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Utajiri wa mbinguni ni wa milele na mungu wake ni Yehova. Utajiri wa duniani ni wa muda na mungu wake ni Mammon. Mammon, ambaye hata Yesu alimtaja katika Injili ya Mathayo 6 na katika Injili ya Luka 16, ni mungu wa uchoyo na utajiri wa dunia hii. Mammon kazi yake ni kufanya watu waliokufa kifedha na walio hai kifedha kuwa maskini wa milele ahera. Yesu Kristo alikuwa maskini, ili tuwe matajiri kupitia umaskini wake, lakini kwa sababu alikuwa na imani ya Mungu katika moyo wake alikuwa tajiri. Hivyo unaweza kuwa na utajiri wa mbinguni hapa duniani, ukiikaribisha amani ya Mungu katika moyo wako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mammon ni mungu wa pesa wa kuzimu anayesimamia mambo yote ya kifedha ulimwenguni. Ni miongoni mwa mashetani saba waliotupwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani kutokea mbinguni akiwemo Ibilisi, Beelzebub, Asmodeus, Leviathan, Amon na Belphegor. Ibilisi ni mungu wa kiburi, Beelzebub ni mungu wa uroho, Asmodeus ni mungu wa zinaa, Leviathan ni mungu wa wivu, Amon ni mungu wa hasira na Belphegor ni mungu wa uvivu. Jukumu la mashetani hawa ni kusimamia kwa uaminifu mkubwa kutokea kuzimu dhambi kubwa saba duniani ambazo ni kiburi, uroho, zinaa, wivu, hasira, uvivu na uchoyo. Dawa ya dhambi hizo ni busara, kiasi, ujasiri, imani, haki, tumaini na upendo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wachawi wanamwabudu Shetani. Lakini Shetani wanayemwabudu si Shetani Ibilisi aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu kuja kuudanganya ulimwengu wote. Ni Shetani roho ya mabadiliko, mabadiliko ya kweli, ya ufahamu kamilia ulimwengu huu ambamo sisi sote tunaishi. Wachawi, kwa maneno mengine, wanaabudu miungu – kama vile Inanna wa Mesopotamia, Isis wa Misri, Asherah wa Kaanani au Belus wa Assyria ambaye ndiye mungu wa kwanza kuabuadiwa kama sanamu duniani – iliyotwaliwa na Shetani tangu misingi ya ulimwengu huu kusimikwa. Dhambi aliyotenda Shetani mbinguni ni ndogo kuliko dhambi wanazotenda wachawi duniani, ijapokuwa dhambi aliyotenda Shetani haitaweza kusamehewa na ndiyo maana Shetani hataweza kuwasamehe wanadamu. Ni jukumu letu kuwaita wachawi wote kutoka Babeli na kuwaleta katika ukweli kama kweli wanayemwabudu ni Shetani Ibilisi, Shetani Beelzebub, Shetani Asmodeus, Shetani Leviathan, Shetani Mammon, Shetani Amon au Shetani Belphegor ambao ni mabingwa wa kiburi, uroho, zinaa, wivu, fedha, hasira na uvivu duniani. Wachawi hawajui, na usipojua waweza kufa bila kujua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wachawi wanaabudu miungu ambayo ndani yake kuna Shetani, aliyesababisha Ibilisi achague mabaya badala ya mema kabla Mungu hajamfukuza mbinguni. Shetani ndani yake kuna Shetani. Huyo Shetani aliyeko ndani ya Shetani, anayeitwa Roho ya Mabadiliko ya Kweli ya Ufahamu Kamili wa Siri ya Uumbaji wa Mungu (kwani ukiijua siri ya uumbaji wa Mungu unakuwa kama Mungu), ndiye anayeabudiwa na wachawi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani alikuwa kiumbe mzuri kuliko wote mbinguni na ulimwenguni. Mungu alimpendelea. Alikuwa mzuri kuliko malaika wote na alikuwa na nguvu kuliko kiumbe mwingine yoyote yule aliyeumbwa na Mungu, akiwemo binadamu. Lakini alipotupwa kutoka mbinguni kuja duniani kama Adamu na Hawa walivyotupwa kutoka bustanini kuja duniani, Shetani alipoteza sifa yake. Alipoteza sifa yake kwa sababu ya dhambi aliyoitenda, dhambi ya kiburi, na kwa sababu ya kuwa mbali na utukufu wa mbinguni. Badala ya kuwa kiumbe mzuri kuliko wote, Shetani akawa kiumbe mbaya kuliko wote. Mungu akaahidi kutokumsamehe, kwa sababu yeye ndiye kiumbe wa kwanza kutenda dhambi mbinguni na ulimwenguni, kwani hakushawishiwa na mtu kumuasi Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yesu alipokuwa msalabani watu wengi walimzunguka. Askari wa Kirumi aliyekuwa na chongo, na mkuki, alikuwa na jukumu la kumtesa Yesu hadi kufa kwa amri ya Pilato. Yesu alipolia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”, yule askari alikurupuka na kumwendea Yesu. Lakini Yesu alishakata roho. Kuthibitisha kama Yesu alishakata roho, askari alimchoma Yesu mkuki kwenye mbavu kwa nguvu zake zote. Mkuki huo ukamtoboa Yesu hadi upande wa pili, ukatoboa hata moyo wake. Askari alipochomoa mkuki, damu na maji viliruka na kupiga jicho lake bovu. Papo hapo askari akapona na kuona vizuri. Alipoona kweli amepona na kuona vizuri, askari alipiga kelele, alipiga magoti na kuomba Mungu amsamehe dhambi zake. Msamaha una nguvu kuliko dhambi. Askari huyo atakwenda mbinguni. Haijalishi umechukia watu kiasi gani. Haijalishi umetesa watu kiasi gani. Haijalishi umeua watu kiasi gani. Haijalishi umetenda dhambi kiasi gani. Mungu anachotaka kutoka kwako, tubu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tukio la Yesu kufa, kufufuka na kupaa kwenda mbinguni bila mabawa ni tukio kubwa kuliko yote yaliyowahi kutokea katika historia ya ulimwengu huu. Naamini, Mungu yupo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu hatakubali kuwa na mtu katika ufalme wake ambaye hatakubali kutawaliwa naye. Usikubali kutawaliwa na Ibilisi, kubali kutawaliwa na Mungu. Ni jukumu letu kuanza kuishi sasa kama vile tutakavyoishi mbinguni. Shetani anataka uwe na hekima ya duniani ili akupumbaze. Lakini hofu ya Mungu ndiyo msingi wa hekima ya kweli. Ukitaka asikupumbaze, pokea Roho ya Mungu kwa kubatizwa. Ukiipokea Roho ya Mungu utajua mambo ya Mungu, ambayo dunia haiwezi kujua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watakatifu wote watanyanyuliwa na wataondoka pamoja na Yesu kuelekea mbinguni, kwa ajili ya ziara ya miaka 1000 katika ulimwengu wa roho; kuanzia dunia ya kwanza ya ulimwengu huo iitwayo Asiyah hadi ya mwisho iitwayo Adam Kadmon, katika mji mpya wa Yerusalemu.

Baada ya milenia, kipindi hicho huku duniani Ibilisi akiwa kifungoni na malaika wake, binadamu wote wenye dhambi wakiwa wamekufa, Yesu na watakatifu wote atarudi kwa ajili ya ufufuo wa pili; na kama mfalme wa ulimwengu wote milele.”
Enock Maregesi