Makamanda Quotes

Quotes tagged as "makamanda" Showing 1-3 of 3
Enock Maregesi
“Radia Hosni alikuwa na bahati kuliko watu wote duniani. Frederik Mogens alipofika katika helikopta na kukuta Murphy na Yehuda wakihangaika kuutafuta mwili wa Radia, hakushangazwa na walichomwambia. Kwa sababu alijua nini kilitokea. Radia alikutwa akipumua kwa mbali. Hivyo, Debbie na marubani walimchukua na kumpeleka Mexico City haraka ilivyowezekana. Black Hawk waliyokuwa wakiishangaa ilikuwa ya DEA. Lakini si ile waliyokwenda nayo Oaxaca. Ilikuwa nyingine ya DEA, iliyotumwa na Randall Ortega kuwachukua Vijana wa Tume na kuwapeleka Mexico City haraka ilivyowezekana. Black Hawk waliyokwenda nayo Oaxaca ndiyo iliyomchukua Radia na Debbie na kuwapeleka Altamirano (hospitali ya tume) mjini Mexico City. Mogens angekwenda pia na akina Debbie; lakini alibaki kwa ajili ya kumlinda El Tigre, na mizigo yake, na baadhi ya makamanda wake wachache. El Tigre angeweza kutoroka kama angebaki na polisi peke yao, na Mogens hakutaka kufanya makosa.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Watu wanaohatarisha maisha yao kwa kudharau sheria wakati mwingine hawatakiwi kudharauliwa. Ni sawa na mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake. Wana uwezo wa kufanya chochote. Serikali ya Meksiko ilipokataa kukidhi matakwa ya El Tigre ya kubadili katiba ya nchi – kuondoa kipengele cha mkataba wa kubadilishana watuhumiwa na washtakiwa – ili akikamatwa asipelekwe Marekani ambako atafungwa na kufia gerezani, El Tigre aliilaani Serikali ya Meksiko. Kujibu mapigo, ya laana ya maluuni, Serikali ya Meksiko ikawakabidhi makamanda 7 wa Kolonia Santita kwa mamlaka za Marekani, na kuongeza juhudi za kumsaka El Tigre mpaka nje ya Amerika ya Kusini na Kaskazini. El Tigre, kuikomoa serikali na kuwalipia kisasi makamanda wote waliouwawa na kufungwa na shirikisho, akamuua Mwanasheria Mkuu wa Serikali (PGR) na maafisa 7 wa Jeshi la Polisi la Nchi (PJF) kulinganisha idadi ya makamanda wake waliopelekwa Marekani – halafu 'akapotea', kabisa; baada ya kutangaza vita na Serikali ya Meksiko!”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Ndege ya Kolonia Santita, Grumman Gulfstream III, tofauti na ndege alizokuwa akitumia Panthera Tigrisi na makompade wake wa karibu, ilifanya kazi kubwa katika mgogoro wa Kolonia Santita na Tume ya Dunia. Dar es Salaam Grumman ilipomchukua kachero Giovanna Garcia wa Kolonia Santita, baada ya ndege hiyo kutumwa na makamanda wa Kolonia Santita wa Copenhagen, ilimpeleka Paris nchini Ufaransa kuhudhuria kikao cha siri cha CS-Paris. Katika kikao hicho yeye na wenzake wakapanga mauaji ya Kamanda John Murphy Ambilikile, kwa kusuka mbinu kamambe za kumteketeza, kabla ndege yake haijafika Copenhagen. Giovanna akashiriki pia kupeleka taarifa za Murphy duniani kote katika matawi yote ya Kolonia Santita, Urusi ikiwemo, ambapo Murphy alitekwa nyara na CS-Moscow. Baada ya 'mauaji' ya Murphy, Grumman iliwapeleka baadhi ya maadui waliohusika na mauaji hayo Mexico City katika makao makuu ya Kolonia Santita; kisha ikarudi Copenhagen kumchukua kiongozi wa CS-Copenhagen, Regner Steiner Valkendorff, na Kachero wa Kolonia Santita Delfina Moore.”
Enock Maregesi